Utu wa Binadamu
Thamani ya asili ya kila mtu; inapaswa kuheshimiwa bila masharti.
Haki za Binadamu: Msingi wa Amani na Maendeleo Endelevu.
Haki za binadamu ni haki za msingi ambazo kila mtu anastahili kwa sababu ya kuwa binadamu — kuishi kwa heshima, bila ubaguzi, na kulindwa dhidi ya vitendo vinavyodhalilisha ubinadamu na usawa wao.
Haki zote zimeainishwa katika Mikataba ya Kikanda na Kimataifa, pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sehemu ya Tatu — Haki na Wajibu, Ibara ya 12 hadi 29.
Misingi mikuu inayofafanua jinsi haki za binadamu zinavyoeleweka na kutekelezwa.
Thamani ya asili ya kila mtu; inapaswa kuheshimiwa bila masharti.
Watu wote ni sawa mbele ya sheria na katika kupata haki, fursa na huduma.
Kuzuia ubaguzi kwa misingi ya jinsia, ulemavu, kabila, dini, umri, au hali ya kiuchumi.
Haki ni za kila mtu, kila mahali, na wakati wote, bila masharti.
Haki zote zimeunganishwa; ukiukwaji wa haki moja huathiri nyingine.
Kila mtu ana uhuru wa maoni, dini, kujieleza, kutembea, na kushiriki katika masuala ya jamii.
Serikali inawajibika kulinda, kukuza, na kuhifadhi haki za binadamu; wananchi wana jukumu la kulindana haki na kutoa taarifa za ukiukwaji.
Haki za binadamu zimegawanyika katika makundi kadhaa yanayotegemeana.
Haki zinazolinda uhuru wa mtu binafsi, ikijumuisha haki ya kuishi, uhuru wa kujieleza, uhuru wa kuabudu, haki ya kusikilizwa kwa haki, uhuru wa mawazo, haki ya kushiriki kisiasa, na kulindwa dhidi ya mateso au ukatili.
Haki ya elimu, afya, makazi bora, chakula, kazi yenye staha, hifadhi ya jamii, na kushiriki katika maisha ya kiutamaduni.
Haki zinazohusu ustawi wa jamii kwa ujumla — ikijumuisha haki ya maendeleo, mazingira safi, amani, kujitawala, na ushirikiano wa kimataifa. Haki hizi zinalenga jamii, mataifa na makundi badala ya watu binafsi pekee.
Haki zinazolinda maslahi ya watoto, vijana, wanawake, watu wenye ulemavu, wazee, wafungwa, na wakimbizi. Haki hizi zinasisitiza kujumuisha mahitaji yao maalum katika huduma za jamii, mipango ya maendeleo, na fursa za kiuchumi na kisiasa.
Haki za faragha mtandaoni, ulinzi wa data (taarifa), matumizi salama ya akili bandia (AI), na haki nyingine ibuka zinazotokana na maendeleo ya teknolojia.
Ukiukwaji wa haki za binadamu unaweza kutolewa taarifa kupitia njia zozote zifuatazo.
📞 026 2160360 | 0800 004 004
💬 WhatsApp: 0739 101 910
✉️ complaints@sheria.go.tz